Wakulima wahamasika kujiunga na kilimo rafiki na mazingira

Wakulima wa kijiji cha Machali wilayani Chamwino wahamasika kujiunga na kilimo rafiki na mazingira baada ya kuona wakulima wenzao wamenufaika kwa kupata mazao ya kutosha. Pia mkuu wa wilaya amewashauri wakulima kutumia mbolea za wanyama na mbolea za mimea kama maganda ya karanga ili kuweza kupata mazao ya kutosha. Pia kujiunga kwenye vyama vya ushirika ili kuweza kupata masoko kwa urahisi.

Bofya hapo chini kwa maelezo zaidi:

Advertisements

Athari za Uharibifu wa Misitu katika Kilimo

Shughuli za kilimo katika kijiji cha Ksiongwe wilayani Kilosa zimekuwa zikiathiriwa sana na shughuli za uchomaji mkaa ambazo zimekuwa zikifanyika katika msitu wa hifadhi uliopo katika kijiji hicho.  Uchomaji wa mkaa pamoja na shughuli nyingine haramu katika msitu zimekua zikichangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza gesi joto katika tabaka la hewa na hivyo kuchangia katika kuleta mabadiliko ya tabianchi.

Kwa maelezo zaidi bofya hapa chini

 

Kilimo Rafiki na Mazingira

Zitambue njia za kilimo rafiki na mazingira zitakazokuwezesha kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi katika shughuli zako za kilimo.

Kipeperushi hichi kinatoa ufafanuzi wa njia mbalimbali zinazoweza kutumiwa na mkulima katika maeneo yenye miinuko na kumwezesha kuvuna zaidi huku akikabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Pia kitakupa ufahamu wa faida za kutekeleza kilimo rafiki na mazingira.

Mabadiliko ya tabianchi na wakulima wadogowadogo Tanzania.

Wakulima wadogowadogo nchini Tanzania wamekuwa wakiathiriwa na changamoto za mabadiliko ya tabianchi katika shughuli zao za kilimo na kuwapelekea kuzalisha mazao kidogo bila kupata faida. Zipo njia mbalimbali za kilimo ambazo zitawawezesha wakulima kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kuwawezesha kuongeza uzalishaji na kujiongezea kipato bila kuongeza gesi joto katika tabaka la hewa la nchi.

Kwa maelezo zaidi, sikiliza mahojiano hapo chini.